Alisson apona majeraha huku Liverpool ikiendelea kusubiri hatma ya ubingwa.
Alisumbuliwa na tatizo kidogo kwenye mazoezi na baadae akakosa mchezo wa mwezi uliopita uliouiondoa liverpool nje ya michuano kwa kupigwa 3-2 na Atletico Madrid na kupoteza sifa ya kuwa bingwa mtetezi.
Adrian alichukua nafasi ya mbrazili huyo ambaye alisababisha magoli mawili ya Marcos Llorente yaliyoleta jumla ya magoli 4-2 na wahispaniola kutinga hatua ya robo fainali.
Alisson amerusha video inayomuonyesha akirukaruka na kufanya mazoezi mbalimbali ikithibitsha kuwa nyota huyo amepona nyonga yake.
kwa sasa kipa huyo na wachezaji wenzake wanafanya mazoezi kila mmoja nyumbani kwake kwa kuepuka msongamano na kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.